1232 22nd St. NW Washington D.C 20037
ubalozi@tanzaniaembassy-us.org
202-939-6125 202-884-1080 202-884-1083 (Visa)
Embassy of Tanzania, DC

Ambassador Liberata Mulamula

Her Excellency
Ambassador
Liberata Mulamula
Head of Mission

Utangulizi

Watanzania wenzangu,

Karibuni Ubalozi wa Tanzania.
Ubalozi wa Tanzania hapa Marekani unapenda kuwatangazia rasmi juu ya ukurasa huu umeanzishwa kwa Watanzania waishio Marekani, na Wamarekani wenye asili ya Tanzania.

Nchi ya Marekani ni Kubwa na ni vigumu Maafisa wa Ubalozi kumfikia kila Mtanzania huko aliko. Hivyo tunawaomba Watanzania wanaoishi Marekani kujiandikisha majina na anuani zao katika ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwakupitia tovuti. Kwa bahati, TEKNOHAMA sasa inatuwezesha kuwasiliana hata bila kutembeleana. Kwenye ukurasa huu kuna eneo la jumla la kujiandikisha, ili ubalozi ujue mlipo na namna ya kuwafikia na kuwasiliana nanyi. Lipo pia eneo la Watanzania kuonyesha kujiandikisha ujuzi wa fani zao za kila aina walizonazo. Pia, zipo habari za matukio na taarifa zinazowahusu Watanzania.

Ndugu zangu Watanzania, Ubalozi huu unaamini kuwa wapo Watanzaina wengi waliosoma na kubobea kwenye fani mbalimbali za kitaaluma. Huu ni utajiri wa nguvu-kazi ya taifa letu, na hazina inayoweza kutumiwa na serikali yetu, au makampuni binafsi yanayowekeza nchini mwetu.

Tunawaomba watanzania wote wachukue nafasi hii muhimu ya kuwa karibu na nchi yao kwa kushiriki kikamilifu kujenga maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Taifa la Tanzania.

Ubalozi huu upo kwa ajili yenu na tungependa tuunganishe jumuiya ya Watanzania waliopo Marekani kimtandao na tutoe fursa ya kuchangia mambo ya kimsingi na kimaendeleo kwetu na kwa nchi yetu.

Ubalozi upo kwa kila Mtanzania kutoa maoni yake jinsi gani Watanzania walioko Marekani wanaweza kuchangia maendeleo ya nchi yetu kwa kutumia maarifa na uzoefu wao wa kuishi kwenye taifa hili kubwa lenye uchumi mkubwa duniani.

Ubalozi unaamini kwamba wote kwa pamoja tukishirikiana tutaijenga nchi yetu.

Nyumbani ni Nyumbani
Liberata Mulamula
Balozi