1232 22nd St. NW Washington D.C 20037
ubalozi@tanzaniaembassy-us.org
202-939-6125 202-884-1080 202-884-1083 (Visa)
Embassy of Tanzania, DC

Utaratibu wa Kubadili Cheti Cha Chanjo Cha Kimataifa

 1. Nenda na cheti cha zamani na hati ya kusafiria katika mojawapo ya vituo hivi

  • Bandari: Dar es salaam, Tanga, Kigoma, na Mwanza
  • Viwanja vya ndege: Dar es salaam, Mwanza, na Kilimanjaro
  • Mipakani: Tunduma, Kasumulu, Mtambaswala, Tarakea, Holili, Horohoro, Namanga, Mutukula, Rusumo, Sirari na Isaka
  • Hospitali ya Mnazi Mmoja
 2. Utajaza fomu ya kubadili cheti cha chanjo cha kimataifa (utaipata kituoni au kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz)
 3. Cheti chako kitahakikiwa na kama ni halali utalipia Tsh.5000 (Mtanzania), dola 10 za Kimarekani (asiyekuwa Mtanzania). Baada ya kukamilisha malipo utapewa cheti kipya
 4. Kama umepoteza cheti cha zamani, nenda na taarifa ya upotevu kutoka polisi na hati ya kusafiria
 5. Kama una cheti ambacho sio halali, mtumishi wa afya atakufanyia tathmini ya ulazima wa kuchanja ndo akupatie cheti kingine
 6. Endapo utashindwa kubadilisha kwa sababu ya kuwa nje ya Tanzania ifikapo 31/03/2017, utaruhusiwa kubadili katika kituo cha Afya mpakani wakati unaingia Tanzania
 7. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Dr. Khalid Massa namba 0713413699 au Remidius Kakulu namba 0767285692