1232 22nd St. NW Washington D.C 20037
ubalozi@tanzaniaembassy-us.org
202-939-6125 202-884-1080 202-884-1083 (Visa)
Embassy of Tanzania, DC

Tangazo La Zoezi La Pasipoti Katika Miji Ya Wichita Na Kansas City

TANGAZO LA ZOEZI LA PASIPOTI KATIKA MIJI YA WICHITA NA KANSAS CITY

Ubalozi wa Tanzania Washington DC, unapenda kuwatangazia Watanzania wote wanaoishi katika miji ya Wichita na Kansas city kuwa, zoezi la kushughulikia maombi ya kubadilisha pasipoti za zamani, litafanyika katika miji iliyotajwa hapo juu kuanzia tarehe 10/10- 14/10/2014.

Aidha, Ubalozi unawakumbusha Watanzania wanaoishi katika miji na vitongoji jirani na miji ya Wichita na Kansas City kama vile Missouri, Iowa, Nebraska, Arkansas, Kentucy, Oklahoma, Texas na Colorado kuitumia fursa hii muhimu kushughulikia maombi ya kubadilisha pasipoti zao.

Ubalozi unapenda kusisitiza kuwa, watoto wote waliozaliwa Nchini Marekani kwa wazazi ambao aidha wote ni Raia wa Tanzania au hata kama mzazi mmoja tu ndiye Raia wa Tanzania kuwa wanayo haki ya kuomba na kupewa pasipoti ya Tanzania. Kwa maana hiyo, ni jukumu la wazazi wa watoto wenye sifa hii kuhakikisha kuwa wanawaombea watoto wao pasipoti ya Tanzania wakati wa zoezi hili.

Kila atakayelisoma Tangazo hili, amuarifu Ndugu, jamaa au rafiki yake wa karibu. Taarifa ya saa na mahali ambapo zoezi hili litakapofanyikia, zitatolewa kupitia kwa Wenyeviti wa Jumuia za Watanzania katika miji na maeneo niliyoyataja.

Imetoleawa na Kitengo cha Huduma za Konseli.
Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Tarehe 16.09.2014.